
Dar es Salaam. Mwanasheria Mkuu mstaafu, Jaji Mark Boman amekitaka Chama cha Mapinduzi (CCM) kuachana na msimamo wake wa muundo wa Serikali mbili na kwamba, wawaachie wananchi waamue.
Pia, Jaji Bomani alisema anasikitishwa na madai yanayoelezwa na baadhi ya viongozi, tena anao waheshimu kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Katiba, Jaji Joseph Warioba ni muumini wa Serikali tatu kwamba ni upuuzi, kwani yeye siyo wa kwanza kutaja muundo huo. (JM)
Akitoa maoni yake kuhusu Rasimu ya
Pili ya Katiba, Jaji Bomani alisema licha ya kwamba yeye ni mwanaCCM,
anaona Serikali tatu ni muhimu kwani ndiyo suluhisho la migogoro ya
Muungano.
Alisema amekuwa mwanaCCM tangu mwaka 1960, lakini hajatetereka ingawa wakati mwingine amekuwa haridhiki na baadhi ya mambo.
"CCM ni chama tawala, chenye wanachama
wengi kuliko chama kingine cha siasa, hivyo ina jukumu la kutoa uongozi
na kuacha baadhi ya mambo wananchi waamue," alisema Jaji Bomani na
kuongeza:
"Nikisikia kitu kama wanaCCM kulishana
kiapo ili wapinge Serikali tatu nafadhaika sana. Haya yote ya nini!
Waachieni wanachama wenu waamue wanachokitaka kuliko kuwashinikiza
kufanya uamuzi mnaotaka nyie."
Alisema kazi ya chama ni kutoa ushauri
na ushawishi, siyo kutoa shinikizo hivyo ni vyema kuacha kuwa na
msimamao wa Serikali mbili, kwani kilichopendekezwa na Tume ndiyo
sahihi. CHANZO, MAWANANCHI
Jaji Bomana alihoji kama CCM ilitaka Serikali mbili, iwapo waliwahi kuwapa wanachama wao elimu juu ya muundo huo.
"Itakuwa siyo uongozi bora kwa wana
CCM kushinikiza kupigia kura mfumo wa Serikali mbili kwa namna ya
vitisho. Nashauri wanachama na wananchi waachiwe uhuru bila kushinikizwa
na mtu," alisema Jaji Bomani.