Picha
juu na chini ni magari ya kuzolea taka ngumu ya kampuni mbalimbali
yakiwa kwenye foleni ya kuingia Dampo la Pugu Kinyamwezi ambalo miundo
mbinu yake ni mibovu na kupelekea zoezi hilo kuchukua zaidi ya siku 4
mpaka kufanikisha kufikia eneo maalum la kumwagia taka ngumu.
.Ni kutokana na kukwama kwa magari ya taka kwenye Dampo la Pugu
.Siku ya tatu sasa magari ya taka yamekwama
Na.Mwandishi wetu, MOblog
MIUNDOMBINU
mibovu katika Dampo kuu la jiji la Dar es Salaam Pugu Kinyamwezi
imesababisha magari makubwa ya kuzoa na kumwaga taka kukwama kwa muda wa
siku tatu na kupunguza ufanisi wa kuzoa taka katika mkoa wa Dar es
Salaam, MOblog inaripoti.
Mtoa
taarifa wetu ambaye hakutaka kutajwa kwenye blogu hii, amesema kwamba
uongozi wa Dampo Pugu umeshidwa kuweka utaratibu mzuri na kukarabati
miundombinu ya dampo kwa muda mrefu na kusababisha msongamano mkubwa
wakati wa kwenda kumwaga taka katika sehemu hiyo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari wa MOblog jana asubuhi, mtoa taarifa (Jina
linahifadhiwa) amesema kwa muda wa wiki mbili sasa umwagaji wa taka
katika dampo hilo siyo mzuri kabisa na inaweza kufika miezi kadhaa tangu
dampo hilo lianze kuelemewa na uchafu kutoka kila kona ya jiji la Dar
es Salaam.
“hali
ni mbaya katika dampo la pugu kwa miezi kadhaa sasa na uongozi wa dampo
wameshidwa kufanya kazi kwa tija na kusababisha usumbufu mkubwa kwa
watumiaji wa dampo katika jiji la Dar es Salaam,’ amesema mtoa taarifa.
Amesema
magari makubwa aina ya (Bulldozers) hayawafanyi kazi kabisa na
kusababisha kukwama kwa kazi ya kumwaga taka katika dampo la Pugu
Kinyamwezi na msongamano mkubwa wa magari. Mtoa
taarifa anasema kuwa kutokana na matatizo hayo katika dampo la Pugu
imesababisha baadhi ya taka kuoza kabisa na kuleta harufu kali kwa
wakazi wa karibu wa dampo hilo na tishio la magonjwa ya mlipuko ni
kubwa. “kutokana na tatizo hili katika dampo la hapa
Pugu hali za kiafya kwa wakazi wa karibu wa eneo ni ya hatari na
magonjwa ya mlipuko yako mbioni kutokea,” aliongeza.

