| WATU watatu akiwemo Mkuu wa
Upelelezi wa Wilaya ya Newala, ASP-
Nurdini Kassim Seif (38) wamefariki
dunia kufuatia ghasia zilizojitokeza
jana ((12.1.2014) katika Kijiji cha
Kiduni Kata ya Mtonya Tarafa na
Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara.
Hayo yamebainishwa leo na Issa
Mnilota (ACP) ofisini kwake kwa niaba
ya Kamanda wa polisi Mkoa wa
Mtwara Zelothe Stephen wakati
alipokuwa akiwasilisha taarifa
kuhusiana na tukio hilo kuwa, tukio
limetokea mnamo majira ya saa 16:45.
Aidha, amewataja marehemu hao kuwa
mwananchi mmoja aliyetambulika kwa
jina la Hamza Msangaluwa ambaye
amefariki baada ya kupigwa risasi ya
kichwa , Mkuu wa upelelezi ASP-
Nurdini Kassim Seif (38) na F.8106 DC
Rogert ambapo wote walikufa papo
hapo baada ya kushambuliwa sehemu
mbalimbali ikiwemo kifuani, tumboni,
mapajani na miguuni kufuatia vurugu
hizo.
Aidha waliyoshmbuliwa ni F.5339 (33)
na PC Issaya (34) ambapo PC Issaya
amejeruhiwa vibaya sehemu ya paja
ambapo kwa sasa yuko katika
Hospitali ya Wilaya ya Newala kwa
matibabu zaidi.
Vurugu hizo zimetokea nje kidogo ya
Mjini wa Newala umbali wa km 5
barabara ya Newala ? Mtwara ambapo
jambazi mmoja akiwa na silaha
inayosadikiwa kuwa SMG alikwenda
kituo cha mafuta cha Camel akiwa
amebeba galoni na kununua mafuta ya
Tshs. 2500/= na kuweka kwenye
galoni alokuwa amebeba.
Mara baada ya kupatiwa mafuta hayo
aliingia ndani ya jingo la kituo hicho
na kuwataka wahudumu wampatie
mauzo ya siku mbili yaliyofanywa
kituoni hapo ambapo wahudumu
walimjibu kuwa hawana fedha, fedha
zote zimechukuliwa ndipo alipotoa
silaha aliyokuwa ameficha ndani ya
koti alilokuwa amevaa na
kuwalazimisha watoe fedha. Kufuatia hatua hiyo jambazi huyo
alianza kupekuwa na kuona fedha
zilizokuwa uvunguni mwa meza ya
kituo hicho na hatimaye alifanikiwa na
kuweka fedha hizo ndani ya mfuko wa
koti alilokuwa amevaa na kikumbilia
vichakani?.Alisema Mnilota.
Hata hivyo wahudumu hao walianza
kupiga kelele na kuomba msaada
kutoka kwa wananchi ndipo wananchi
walianza kujitokeza na kuanza
kumkimbiza na wakiendelea kumfatilia
kwa nyuma, jambani huyo alianza
kuwafyatulia risasai lakini wananchi
waliendelea kumkimbiza kiasi cha
umbali wa km 8 na kuingia kwenye
kichaka.
Alisema kuwa, polisi nao kwa muda
huo walikuwa tayari wamepata raarifa
na kuelekea na eneo la tukio ambapo
jambazi huyo akiwa amejificha kwenye
kichaka alifanikiwa ndipo akafanikiwa
kumpiga risasi mwananchi huyo
mmoja ambaye ni marehemu baada ya
kubaini alipokuwa amejificha jambazi
huyo hata hivyo jirani akiwepo Mkuu
huyo wa upelelezi.
Aidha, jambazi huyo amefanikiwa
kutoweka gizani na kuacha helment,
koti, raba moja na mzula aliokuwa
amevaa na mwili wa marehemu Hamza
Msangalukwa tayari umechukuliwa na
ndugu zake kwa mazishi na miili
mingine bado imehifadhiwa katika
Hospitali ya Wilaya hiyo kwa taratibu
zingine.
Alisema kuwa, jeshi la polisi linatoa
shukrani kwa wananchi wa Kijiji na
Vijiji vya jirani na watendaji wote wa
Halmashauri hiyo kwa ushirikiano
walioutoa na wanaoendelea kuutoa
kwa jeshi la polisi.
Aidha, jambazi huyo amefanikiwa
kuondoka na kiasi cha fedha Tshs.
3,299,180/= ya mauzo toka katika
kituo cha mafuta cha Camel na
masako mkali wa kumsaka jambazi
huyo unafanyika na watatoa taarifa
zingine zitakazo patikana.
Pia jeshi la polisi Mkoani hapa linatoa
rai kwa wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano utakaowezesha kuwabaini
na kuwakamata wale wote
waliohusika na tukio hilo. |