
Eden Hazard alifunga bao la kwanza Chelsea ikiilaza Hull City
MSHAMBULIAJI Eden Hazard 'amelipa'
fadhila kwa kocha Jose Mourinho baada ya kuifungia Chelsea bao katika
ushindi wa 2-0 dhidi ya Hull City na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu ya
England jioni ya leo.
Huku ikiripotiwa kwamba tayari Paris
St Germain wanamtaka kiungo huyo Mbelgiji wa Chelsea, Mourinho amesema
wiki hii kwamba hatakubali hata ofa ya Pauni 100,000.
Alifunga bao lake dakika ya 57 kabla
ya Fernando Torres kufunga la pili dakika tatu kuelekea mwishoni mwa
mchezo. Chelsea imetimiza pointi 46 baada ya kucheza mechi 21 ikiwa juu
ya Arsenal yenye pointi 45 na Manchester City pointi 44, ambazo
zimecheza mechi 20