Samuel Eto'o amekuwa mchezaji wa nne kuifunga Machester Utd mabao 3 ( Hat Trick ) kwenye ligi kuu ya England.
Eto'o
ameungana na kina Romelu Lukaku,David Bentley na Dirk Kuyt kuifunga Man
Utd Hat Trick baada ya kufunga mabao yote matatu kwenye mchezo ambao
Chelsea imeifunga Man Utd mabao 3-1 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.
Hat Trick ya Eto'o ilikuwa ni ya 25 kwa wachezaji kutoka Barani
Afrika kwenye ligi kuu ya England akiungana na wakali kama Mghana Tony
Yeboah,Wanigeria Nwankwo Kanu,Yakubu Aiyegbeni,Peter Odemwingie,Wa-Ivory
Coast Didier Drogba na Salomon Kalou wengine ni Emmanuel Adebayor,Peter
Ndlovu bila kumsahau raia mwingine wa Cameroon mshambuliaji wa zamani
wa West Bromwich Albion Somen Tchoyi.NA SHAFFIH DAUDA
