![]() |
| Rais Jakaya Mrisho Kikwete Akimpa Pole Mke Wa Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu Bi Mariam Alipotembelea Na Kwenda Kuwafariji Wafiwa Nyumbani Kwa Marehemu Sinza Mori Dar Es Salaam |
Mariam, ambaye ni mke wa pili wa Balozi Sepetu
aliyefunga naye ndoa ya kimila mwaka 1982, alisema mumewe enzi za uhai
wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi, ikiwamo ya Ubalozi
Urusi na kwamba, kwa kutambua mchango wake, Rais wa Zanzibar, Dk Ali
Mohamed Shein aliagiza agharimiwe matibabu lakini hakuna hatua
zilizochukuliwa.
Akizungumza jana nyumbani kwake, Sinza Dar es
Salaam, Mariam alisema alijaribu kuwasiliana na Wizara ya Afya
Zanzibar, lakini hakupata ushirikiano aliopata, aliamua kumsafirisha
mumewe huyo kutoka Zanzibar hadi Dar es Salaam Oktoba 24, mwaka huu na
kumpeleka Hospitali ya TMJ Mikocheni.
“Nishukuru watoto wake wote waliungana na
kushiriki kikamilifu kumuuguza baba yao, wakishirikiana na ndugu na
jamaa zetu wachache. Kwa kweli jambo hili limenihuzunisha sana nafikiri
hakupata huduma ya kutosha,” alisema.
CHANZO: MWANANCHI
CHANZO: MWANANCHI

