![]() |
Na Eleuteri Mangi- MAELEZO, Mtwara.
Mradi
wa uzalishaji gesi asilia umeonesha kuwa ni kichocheo kikuu na muhimu
katika kuleta na kuinua sekta ya viwanda nchini kwa manufaa ya taifa na
wananchi wake.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mizengo Pinda wakati wa ziara ya kikazi ya siku mbili katika mikoa ya
Lindi na Mtwara hivi karibuni alipokuwa akitembelea mikoa hiyo kwa lengo
la kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa bomba la kuisafirisha gesi
asilia kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam.
“Ujenzi
wa viwanda vya vya saruji vya MEIS kilichopo kijiji cha machole mkoani
Lindi na Dangote kilichopo kijiji cha Msijute mkoani Mtwara unaoendelea
ni dalili nzuri na njema kwa nchi na maendeleo ya na watu wake” alisema
Waziri Mkuu Pinda.
Ujenzi
wa viwanda hivi unaoendelea umefikia hatua mbalimbali ni matokeo ya
kugunduliwa gesi asilia katika mikoa hiyo ambapo itakuwa ndio chanzo
kikuu cha nishati ya umeme katika viwanda hivyo.
Waziri
Mkuu Pinda alisema kuwa viwanda hivi vitanufaika na umeme wa kuendeshea
uzalishaji wa saruji katika viwanda hivyo ambao chanzo chake kikuu ni
gesi inayopatikana katika mikoa hiyo.
Ili
kuhakikisha viwanda hivyo vinapata umeme wa uhakika Waziri wa Nishati
na Madini Prof. Sospeter Muhongo alisema kuwa gharama ya kuunganisha
umeme kwa wananchi nchini imepungua katika maeneo mbalimbali nchini.
Prof.
muhongo alisema kuwa kwa sasa maeneo ya vijiji vyote vya mikoa ya
Mtwara na Lindi wamepewa ofa maaluum ya kuunganishiwa umeme kwa gharama
ya sh. 99,000/= za kitanzania ofa ambayo itaisha mwezi Juni mwa huu
ikilinganishwa na gharama ya mwanzoni ambapo nchi nzima wananchi waishio
vjijini bado wanaendelea kuunganishiwa umeme kwa sh. 177,000/=.
Wananchi
wa maeneo hayo wamehimizwa kuchangamkia fursa hii iliyotolewa na
serikali ili kuboreha maisha yao hasa katika karne hii ya sayansi na
teknolojia.
Waziri
Pro. Muhongo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa wananchi wa mikoa ya
Mtwara na Lindi wanaoishi karibu na bomba la kusafirishia gesi kutoka
Mtwara kwenda Dar es salaam wamepunguziwa zaidi gharama ya kuunganisha
umeme kwa sh.27, 000/= za kitanzania.
Muhongo amesisitiza kuwa hakuna serilkali yeyote duniani inayotoa huduma ya kuunganishiwa umeme kwa bei ndogo kama hii.
Waziri
Muhongo amaeendelea kusema kuwa wananchi waishio mijini nao wamepewa
fursa hiyo ya kujihakikishia kuunganishiwa nishati hiyo kwa gharama ya
sh. 330,000/= za kitanzania.
Kutokana
na uhakika wa nishati hiyo katika viwanda vya saruji vya MEIS na
Dangote, wakazi wa maeneo yanayozunguka viwanda hivyo na watanzania kuwa
ujumla watanufaika na kujengwa viwanda hivyo ambapo zaidi ya wananchi
70000 wataajiriwa.
Naye
Mkurugenzi Mendaji wa Kiwanda cha saruji cha MEIS Merea Barabuu alisema
kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kukamilika mwaka huu ifikapo Desemba
kwa kuwa vifaa vyote vimekamilika na vipo tayari.
Barabuu
alisema kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha takribani tani 500
hadi 700 kwa siku ambapo kwa mwaka ni sawa na tani 200,000 hadi 250,000
ambapo malighafi zote za kuzalisha saruji zinapatikana ndani ya mkoa wa
Lindi.
Katika
ziara hiyo Waziri Mkuu katika msafara huo aliambatana Mke wake Mama
Tunu Pinda,Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Hawa
Ghasia, watumishi wa wizara ya Nishati na Madini, watendaji wa shirika
la TPDC, viongozi wa shirika la umeme TANESCO na wabuge wa maeneo ya
mikoa hiyo.
|
