
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan,
amewafuta kazi makamanda wake wakuu wa jeshi ,na kufanya mabadiliko
ambapo amemteuawa mkuu wake wa ulinzi, wakuu wa majeshi ya anga na
majini .
Hakuna sababu iliyotolewa kuhusu hatua hiyo .
Mkuu wa mpya wa majeshi Alex Badeh, anatoka kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi la Nigeria limekuwa likihangaika
kudhibiti uasi wa kundi la kiislam la , Boko Haram, ambalo limekuwa
likiendesha harakati zake zaidi katika maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa
nchi