Watu nchini Israel leo wanaanza
kipindi kifupi cha maombolezi kufuatia kifo cha waziri mkuu wa zamani
Ariel Sharon aliyefariki akiwa na umri wa miaka 85 baada ya miaka 8 ya
kuwa hali mahututi.
Wananchi watatoa heshima zao za mwisho kwa mwili wake Jumapili kabla ya kuzikwa Jumatatu.
Viongozi wa dunia wametoa rambi rambi
zao kwa Sharon, mtu aliyepigana katika vitaa vikuu vinne kabla ya
kuingia katika ulingo wa siasa.
Lakini aliwaacha wapalestina wengi waliomuona kama adui wao wakiwa na hamaki.
Mkuu wa kituo cha afya cha Sheba mjini
Tel Aviv alithibitisha kifo cha Sharon, Jumamosi mchana siku ya Sabato
kwa wayahudi, zaidi ya wiki moja baada ya taarifa kutolewa kuhusu afya
yake kuzorota.
Mmoja wa wanawe Sharon,Sharon, Gilad Sharon, alisema kuwa babake amekwenda wakati alipoamua mwenyewe kwenda.
Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe
Michelle Obama, wamesema Sharon, alikuwa kiongozi aliyejitolea
kuwahudumia watu wa Israel.
Rais Shimon Peres, mwandani mkuu wa
Sharon japo alikuwa hasimu wake wa kisiasa aliyejiunga na serikali ya
Muungano na Sharon mwaka 2001, alisema Sharon alikuwa mtu mwema
aliyepigania watu wake na kuwapenda na kuwa watu pia walimpenda.
Wadhifa wa Sharon kama waziri mkuu
ulifika kikomo baada ya kupatwa na kiharusi na kisha kuwa katika hali
mahututi kwa miaka minane tangu mwaka 2006.
Wakati huu wote alikuwa anatumia mashine kupumua na mirija kulishwa chakula.
Kabla ya hali ya Sharon kuzorota
aliongoza jeshi la Israel kuondoka katika ukanda wa Gaza ili kupunguza
taharuki kati ya Israel na Palestina
