![]() |
| Droo ya michuano ya kombe la FA imefanywa kwa mechi za mchujo wa raundi ya tano.
Chelsea wamepangiwa kucheza na Manchester City katika mchezo unaotazamiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu. |
Droo kamili:
-
Manchester City v Chelsea
-
Sheffield United au Fulham v Nottingham Forest au Preston North End
-
Arsenal v Liverpool
-
Brighton & Hove Albion v Hull City
-
Cardiff City v Wigan Athletic
-
Sheffield Wednesday v Charlton Athletic
-
Sunderland v Southampton
-
Everton v Swansea City
Chelsea ambao wamefuzu kwenye raundi
ya tano kwa kuiondosha Stoke City katika mchezo ambao ulimalizika kwa
ushindi wa bao moja kwa bila.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho akizungumza punde
baada ya droo hii amesema, "Iwapo unataka kuwa bora lazima ucheze na
timu bora."
Nao Manchester City wao walijikatia tiketi ya kufuzu michuano hiyo hatua ya tano kwa kuiadhibu Watford kwa mabao 4-2.
Liverpool wao watakuwa wageni wa Arsenal kwenye mchezo wa raundi ya tano.
Roberto Martinez ataiongoza Everton kukutana na
timu yake ya zamani ya Swansea, ilihali Sunderland wao watacheza na
Southampton ikiwa ni mechi liyokutanisha timu zote za ligi ya England.
Cardiff watakuwa nyumbani kuwakaribisha Wigan na
Hull watacheza na Brighton. Sheffield Wednesday watapamabana na wenzao
walioko kwenye ligi ya Championship, Charlton FC.
Mechi zote zitachezwa jumamosi na jumapili ya tarehe 15 na 16 mwezi wa pili.
Mshindi wa mechi kati ya Fulham ama Sheffield
United atapambana na mshindi kati ya Nottingham Forest au Preston kwenye
hatua ya raundi ya tano ya kombe hilo ambalo fainal yake itachezwa
kwenye uwanja wa Wembley.
