![]() |
| Namnukuu Balozi ‘Ninazo taarifa nyingi ila ni kama mwezi uliopita alikamatwa Mwanaume, ni Wanaume waliokamatiwa Guangzhou,
mtu wangu aliekua anafatilia pia amekuja leo January 9 2014 asubuhi na
kuniambia hakuna taarifa zozote kuhusu Jackline Patrick Cliff’ Kama ni Macao wangetuandikia moja kwa moja, Macao na Hongkong wangetuandikia moja kwa moja na kama wangekua wamewasiliana na balozi wetu wa heshima kule Hongkong pia wangetuandikia, Wachina mtu yeyote wanaemkamata ambae anatumia hati ya kusafiria ya Tanzania wanamuhusisha kama raia wa Tanzania kwa hiyo wanajulisha ubalozi wake labda mtu mwenyewe aseme ni wa taifa jingine, watatuandikia hivyohivyo nakueleza…..’ Baada ya hayo maelezo ya Ubalozi wa Tanzania huko China, maswali yanabaki…. Jackie Cliff yukwapi? mbona marafiki wanasema hawampati kwenye simu? na huyu Mtanzania binti wa miaka 28 aliekamatwa Macao ni nani? |
