Gari ya abiria aina ya Noah imepata ajali mbaya baada ya
kugongana uso kwa uso na Lori,hali iliyopelekea gari hilo la abiria (Noah
kuburuzwa na kutupwa kando kando ya barabara kama lionekanavyo pichani mapema
leo asubuhi,ajali hiyo imetokea kijiji cha Issuna,kijiji cha kwanza kutokea
Manyoni mkoani Singida likielekea Mkoani Dodoma,ajali hiyo ya kusikitisha
ilitokea huku mvua kubwa ikinyesha eneo hilo,hali iliyopelekea kupata msaada
haraka kuwa ya taabu,Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Singida alibainisha
kuwa marehemu wote na majeruhi walikimbizwa hospitali Mkoani Singida,aidha
mpaka sasa imekuwa vigumu kujua idadi kamili ya abiria waliokuwa kwenye gari
hiyo aina ya Noah,hali inayopelekea pia utata wa kutambua majina ya
marehemu.Katika ajali hiyo Dereva wa Lori na Kodakta wake walikimbia eneo la tukio,Polisi
bado inawatafuta kufahamu kwa kina cha chanzo cha ajali hiyo kutokea.
