MBUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA AJIUZULU UDIWANI


DSCF7203
Mbunge,diwani wa viti maalum ambaye pia ni Naibu waziri kivuli wa kazi na ajira kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Wilaya ya karatu Cecilia Paresso akitangaa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kujivua nafasi yake ya udiwani wa viti maalum katika Halmashauri ya karatu nafasi aliyotumikia kwa vipindi viwili toka mwaka 2005 kulia ni Mwenyekiti wa Mkoa chadema Samson Mwigamba
Mbunge wa viti maalum ambaye pia ni Naibu waziri kivuli wa kazi na ajira kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Wilaya ya karatu Cecilia Paresso ametangaza rasmi kujivua nafasi yake ya udiwani wa viti maalum katika Halmashauri ya hiyo kwa vipindi viwili toka mwaka 2005
Akitangaza kujivua wadhifa huo leo jijini Arusha mbele ya waandishi wa habari alisema kuwa haoni sababu ya msingi ya kuendelea kushika nafasi hiyo ya udiwani wakati yeye ni mbunge wa viti maalum hivyo kumuwiya vigumu kushika vyeo wiwili kwa wakati mmoja zenye wajibu ule ule kwa wananchi
“Ndugu wanahabari naomba mfikishe changamoto hii kwa umma wa watanzania ,,mimi binafsi sioni hekima ya kubariki dosari hii ya kimfumo na sheria za nchi yetu ambazo kimsingi ndizo zinazosababisha kutokea kwa mazingira ya mtu mmoja kuwa na nafasi mbili za udiwani kwa wakati mmoja zenye wajibu ule ule na unaotekelezwa kwa watu wale wale “alisema Mh.Cecilia
Alisema kuwa wananchi na wanachama wa chadema karatu wamuelewe pamoja na watanzania kwa ujumla kuwa huo ni uamuzi wa kawaida unaoweza kupimwa kwa mzani wa kawaida katika utawala wa kidemokrasia
Aidha alitoa ahadi ya kuendelea kuwatumikia wanakaratu , watanzania kwa ujumla katika nafasi yake ya Ubunge wa viti maalum ambayo pia inampa fursa ya kuingia kwenye vikao vya halmashauri ya Wilaya ya Karatu
Hata hivyo alisema kuwa kutokana na kujivua kwa nafasi hiyo ya udiwani wa viti maalum tayari taratibu zote za kisheria zimeshakamilika ikiwa ni pamoja na kuwasilisha kwa mkurugenzi barua ya kujivua nafasi hiyo na kufanya kiapo cha kujivua nafasi hiyo katika Mahakama ya ya Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
Pia katika zoezi hilo la kutangaza kujivua nafasi hiyo kwa waandishi wa habari aliandamana pia na Mwenyekiti wa Mkoa(chadema)Samson Mwigamba,Mratibu wa (Bawacha)mkoa Secilia Ndosi
…Jamii Blog…