
Kundi
la wananchi waliojawa na gazabu wamevamia kituo cha Polisi Kibiti
Wilayani Rufiji na kuleta vurugu kubwa kufuatia raia mmoja kufa kwa kile
kilichodaiwa kipigo cha Polisi.
Habari
kutoka Kibiti zinaipasha kuwa kijana aliyefariki kutokana na kipigo
hicho ni Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu
Hospitali ya Muhimbili.
Habari
zaidi zinapasha kuwa hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za
Askari Polisi hao zilizopo jirani na kituo hicho, licha ya juhudi za
Polisi kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika.
Aidha
wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya
Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni
umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.
Hali
inaelezwa kuwa inazidi kuwa tete huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na
jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu hewani kujaribu
kutawanya umati huo wa watu.
Father
Kidevu Blog, ipo eneo la tukio na itakuletea taarifa zaidi na picha
maana hivi sasa ni milipuko ya mabomu tu kwenda mbele.
Source: Father Kidevu Blog